Header Ads

CHADEMA WATANGAZA KUFANYA KONGAMANO LA 'KAHAMA NYEKUNDU'


Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) kimesema kinatarajia kongamano la Kahama Nyekundu yenye lengo la kuhamasisha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa upandaji wa miti zaidi ya 1000 katika halmashauri ya mji wa Kahama.

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kahama,leo Ijumaa Septemba 20,2019  Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Kahama,Jackson Tungu amesema tayari wamekwisha peleka barua ya kuomba kibali cha kufanya zoezi hilo kwa Mkuu wa polisi ambapo wakipata majibu watatangaza ni lini uzinduzi huo utafanyika.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!