Header Ads

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 13 JELA KWA KUMUUA MCHUMBA WAKE

Mahakama ya Cambaodia imemhukumu aliyekuwa gavana wa mkoa wa Taeko, Lay Vannak kifungo cha miaka 13 gerezani baada ya kumpata na hatia ya kuua mchumba wake.

Vilevile, mahakama hiyo imemhukumu aliyekuwa naibu mkuu wa polisi wa mkoa huo Lay Narith, ambaye pia ni nduguye gavana huyo miaka 10 gerezani kwa kushirikiana na yeye kutekeleza mauaji hayo.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, dereva wa Vannak na mfanyikazi wa nyumbani kwa mchumba wake pia walihukumiwa miaka miwli gerezani kwa kuficha ushahidi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!