Header Ads

UCSAF YARAHISISHA MAWASILIANO HALMASHAURI YA USHETU KATA TANO ZANUFAIKA.

Naibu waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuuzindua Mnara huo akiambatana ,na viongozi mbalimbali wa serikali, na Chama katika kijiji cha Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
 KAHAMA
Na Salvatory Ntandu
ZAIDI ya wananchi elfu 50 kutoka kata tano za Halmashauri ya Ushetu Wilayani hapa Mkoani Shinyanga ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano kwa muda mrefu,hatimae wamepata huduma hiyo kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF)

Wakizungumza jana katika hafla ya uzinduzi wa Mnara unaomilikiwa na kampuni ya Vodacom ambao umejengwa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote,walisema kuwa walikuwa watembea umbali kutafuta huduma ya mawasiliano kwa baadhi ya kata zilizo na mawasiliano.

Eliasi Zakaria ni mmoja wa wananchi wa kata ya Nyamilangano alisema,walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya mawasiliano kwa zaidi ya kilomita 100 kufika Kahama Mjini hali ambayo ilikuwa ikikwamisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Nae Ofisa Mjendaji wa kijiji cha Nyamilangano Namana Shabani alisema,walikuwa wanapata shida ya mawasiliano katika kuwaalika wajumbe wa serikali ya kijiji katika mikutano ya maendeleo ambapo njia iliyokuwa ikitumika ni barua au kumfuata nyumbani.

“Tulikuwa tunapata shida kuwaalika wajumbe wa serikali ya kijiji na kata kuhudhuria kikao cha maendeleoa na mfumo ambao tulikuwa tunautumia kuwapa taarifa ilikuwa ni kuwatumia barua ama kuwafuata nyumbani mjumbe mmoja baada ya mwingine hali ambayo ilikuwa inakwamisha shughuli za maendeleo kwenda kwa wakati”alisema Shabani.

Aidha Katibu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF)Justina Mashiba alisema, mpaka sasa zaidi ya Minara 530 imeshafungwa katika kata mbalimbali nchi nzima na zaidi ya wananchi milioni nne wameshanufaika na huduma ya mawasiliano kwa wote vijijini.

Aliendelea kusema kuwa mnamo tarehe 13 mwezi disemba mwaka huu wameshasini mikataba na makapuni ya simu kwaajili ya ujezi  wa minara 173 katika ambazo zinachangamoto ya mawasiliano hapa nchini.

Hata hivyo mwenyekiti wa Mfuko huo Joseph Kilongola alisema wamekuwa walikijenga minara katika kata zenye mvuto wa kibiashara na kuongeza kuwa ifikapo mwaka 2020 kila sehemu zenye changamoto ya mawasilano hapa nchini zitakuwa zimepata huduma hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Vodacom wilaya hapa Jovity Ikate alisema Halmashauri ya Ushetu inajumla ya minara 10 kati hiyo minara miwili imejengwa na Serikali kwa asilimia 100 na kuwataka wananchi wa kata hizo kuchangamkia fursa za kibiashara kupitia huduma ya mawasiliano.

Pia Naibu waziri wa Ujenzi na mbunge wa jimbo la Ushetu Elias kwandikwa alisema kuwa kupatikana kwa Mnara huo kutasaidia kupunguza adha kwa wananchi na watumishi wa Halmashauri hiyo kusafiri umbali mrefu kufua huduma ya mawasiliano.

Aliongeza kuwa serikali kupitia mfuko huo itaendelea kutoa huduma ya mawasiliano katika maeneo yote ambayo yanachangamoto ya huduma ya mawasiliano ili kuongeza chachu ya maendeleo katika kata na vijiji hapa nchini.

MATUKIO KATIKA PICHA:

Meneja wa Vodacom wilaya ya kahama Jovin Ikate akisoma taarifa ya ujenzi wa Mnara huo katika Hafla ya uzinduzi wa Mnara huo katika kijiji cha Nyamilangano.

Katibu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote nchini (UCSAF) akizungumza na Wananchi na viongozi waliohudhuria  Hafla ya Uzindunzi wa Mnara huo ambao umejengwa kwan ufadhili wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote


Baadhi ya wananchi na viongozi waliohudhuria katika Uzinduzi wa mnara huo katika kijiji cha Nyamilangano. 
Mwenyekiti wa Mfuko huo Joseph Kilongola wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) akitoa maelekezo namna Mfuko huo unavyofanya kazi hapa nchini

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu Juma Kimisha akielezea changamoto za mawasilano ambazo walikuwa wanazipata awali kabla ya kujengwa kwa mnara huo.
Viongozi wa Chama na serikali wakishuhudia tukio la uzinduzi wa manara huo jana 
Kulia ni Naibu waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa,katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauria ya Ushetu Michael Matomora na  Mwenyekiti wa Mfuko huo Joseph Kilongola wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) 
Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu Juma Kimisha na Naibu waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa,na Mwenyekiti wa Mfuko huo Joseph Kilongola wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wakifurahia uzinduzi wa Mnara huo.No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!