Header Ads

CHAMA KIKUU CHA MIRAMBO CHAZINDULIWA TABORA,SERIKALI YATOA ONYO KWA WAKULIMA WANAOUZA MBOLEA.


WAKULIMA WA KANDA YA KALIUA WANANCHAMA WA CHAMA KIKUU CHA MIRAMBO WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO.

TABORA
SERIKALI Mkoani Tabora Imewataka viongozi wa chama kikuu cha Ushirika cha Mirambo kuwachukulia hatua kali za kisheria wakulima wote wanaokopa na kuuza pembejeo ikiwa ni pamoja na wanaokiuka taratibu za Ushirika.

Wito huo umetolewa na katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Robert Makungu wakati wa Uzinduzi wa Chama kikuu cha ushirika cha Mirambo kilichopo Urambo mkoani Tabora.

Makungu Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakulima wilayani Humo kukopa pembejeo kwa bei ya juu na kuuza kwa bei ya chini hali inayowafanya wakulima wengi kubaki masikini baada ya mavuno na kuitupia lawama Serikali.

Sambamba na hayo amewaagiza viongozi wa chama cha ushirika Mirambo kutowafumbia macho wanachama wasiofuata taratibu za ushirika ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanachama wengine kujiunga na ushirika ili kuunganisha nguvu katika uzalishaji.

Naye Mrajisi msaidizi tume ya Maendeleo ya Ushirika Sadick Chikira amewataka viongozi wa Chama kikuu cha Ushirika Mirambo kuwaelimisha wanachama pindi inapotokea migogoro na itatuliwe kwa taratibu za kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Dr Julius Ningu amewataka wakulima wa chama kikuu cha Mirambo kuongeza nguvu katika uzalishaji wa zao la Tumbaku ambalo kwa sasa linaingiza pato la taifa kwa asilimia 37% ili kufikia walau asilimia 50%.

Akitoa salamu za wabunge wa Tabora,Mwenyekiti wa Wabunge hao Mama Magreth Sitta amesema kuwa kilio kikubwa cha wakulima kwasasa ni masoko na Pembejeo na kutoa wito kwa chama kikuu cha ushirika Mirambo kuhakikisha kinawasaidia wakulima kuondoa kilio hicho cha muda mrefu.

Awali akielezea ubora wa zao la Tumbaku Mwenyekiti wa wa vyama vya ushirika vya wakulima wa Tumbaku Tanzania Emmanuel Cherehani amewataka wakulima wa zao hilo mkoa wa Tabora kuisimamia Tumbaku kuanzia Shambani hadi Sokoni na kuacha tabia ya kuwaachia wafanyakazi kushughulikia zao hilo.

Tukio la uzinduzi wa Chama kikuu cha Mirambo lilidhaniwa na kampuni ya Petrobena wasambazaji wa Mbolea za Yara ambao wamewahakikishia wakulima hao kupata mbolea kwa wakati na kuwapa mafunzo ya namna bora ya kutumia mbolea kwa kutumia maafisa ugani wao.

Katika mkuutano huo,Ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho ambapo Hassan Magoha alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Ramadani Kalihamwe alichaguliwa kuwa Kaimu mwenyekiti huku wajumbe ni Patrick Mikindo,Mashaka Hamisi,Abisahi Kasele,Thomas Sizya na Mathew Kasagila.

Chama kikuu cha Mirambo ni chama kipya kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Ushirika ambacho kimeanzishwa baada ya wanachama wake wa Urambo na kaliua kujimega kutoka katika chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi  WETCU.

MATUKIO KATIKA PICHA:

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI ROBERT MAKUNGU AKITOA NENO KWA WAKULIMA WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA MIRAMBO.


WANACHAMA WA CHAMA KIKUU CHA MIRAMBO KUTOKA KANDA YA URAMBO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MGENI RASMI.

 MENEJA WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA MIRAMBO AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA KUENDESHA KIKAO CHA KWANZA CHA UZINDUZI WA CHAMA KIKUU CHA MIRAMBO.


KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI ROBERT MAKUNGU AKISAINI KATIKA KITABU CHA WAGENI.

 MRAJISI WA MKOA WA TABORA AKITOA UFAFANUZI KUHUSU NAMNA YA KUENDESHA UCHAGUZI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA.

 WAGENI WAALIKWA KUTOKA TAASISI ZA KIFEDHA,WANUNUZI WA TUMBAKU PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA USAMBAZAJI MBOLEA PETROBENA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO.

MRAJISI MSAIDIZI TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA TAIFA SADICK CHIKIRA AKITOA MISINGI NA MAMBO YA KUZINGATIA KWA WANACHAMA WA CHAMA KIKUU CHA MIRAMBO.

MWENYEKITI WA VYAMA VYA WAKULIMA WA TUMBAKU TANZANIA EMMANUEL CHEREHANI AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO NA KUWATAKA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU TABORA KULISIMAMIA KIKAMILIFU ZAO HILO NA KUACHA TABIA YA KUWAACHIA WAFANYAKAZI KUSHUGHULIKA NA ZAO HILO.

 WAGENI WAALIKWA NA MAAFISA UGANI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MKUTANO.

 BANDA LA PEMBEJEO NJE AYA UKUMBI WA MIKUTANO,WAKULIMA WALPATA NAFASI YA KUULIZA MASWALI NA KUJIBIWA IKIWA NI PAMOJA NA KUPATA ELIMU YA MATUMIZI BORA YA MBOLEA ZA YARA.

 MKURUGENZI MKUU BODI YA TUMBAKU TANZANIA (TTB) DR JULIUS NINGU AKIWASIHI WAKULIMA KUZALISHA KWA TIJA TUMBAKU ILI KUKUZA KIPATO CHA TAIFA.

 MWENYEKITI WA WABUNGGE MKOA WA TABORA MAMA MAGRETTH SITTA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WABUNGE WA TABORA,KIKUBWA AMEZUNGUMZIA KILIO CHA MASOKO NA PEMBEJEO KWA WAKULIMA WA TUMBAKU,NA KUOMBA CHAMA  KIKUU CHA MIRAMBO KUHAKIKISHA KINASIMAMA KUWATETEA WAKULIMA.

 MKUU WA WILAYA YA URAMBO ANGELINA KWINGWA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO NA KUWASIHI WAKULIMA WAZINGATIE KALENDA YA ZAO LA TUMBAKU NA KUHAKIKISHA WAKULIMA WANAPANDA MITI KWA WINGI.

 MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA PETROBENA WASAMBAZAJI WA MBOLEA ZA YARA BWANA PETER KUMALILWA AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO NA KUWAHAKIKISHIA WAKULIMA WA CHAMA KIKUU CHA MIRAM BO WATAPATA MBOLEA KWA WAKATI NA ZENYE UBORA KATIKA KUUMGA MKONO JUHUDI ZA MH RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH JOHN POMBE MAGUFULI.

 MWAKILISHI WA KAMPUNI YA ALLIANCE ONE BWANA MAYUNGA AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO,KIKUBWA AMEWATAKA WAKULIMA MKOANI TABORA KUACHA KUWATUMIKISHA WATOTO MASHAMBANI NA KUPANDA MITI MINGI IKIWA NI PAMOJA NA KUTUMIA MABANI YA KISASA.

ALIYEKUWAMWENYEKITI WA MUDA WA CHAMA KIKUU CHA MIRAMBO BWANA RAMADHANI KALIHAMWE AKISOMA TAARIFA YA CHAMA HICHO NA KWAMBA WAMEJIPANGA KUAPANDA ZAIDI YA MITI MILIONI 4 NA LAKI 6 KWA MSIMU HUU.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!