Header Ads

BOSI WA TAKUKURU DIWANI ATHUMANI AKABIDHI OFISI YA KATIBU TAWALA MKOA WA KAGERA

Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani akiagana na mkuu wa mkoa wa Kagera brigedia jenerali Marco Gaguti katika ukumbi wa mikutano wa halmshauri ya Bukoba leo Oktoba 1,2018.

Picha na Agela Sebastian - 

****
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani amekabidhi ofisi ya katibu tawala katika mkoa wa Kagera ambayo alikuwa akiitumikia kwa takribani miaka miwili kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU.

Akiagana na watumishi wa kada mbalimbali mkoani Kagera leo Oktoba 1,2018 pia ameweka wazi mikakati yake ya muda mfupi,kati na mrefu itakayowezesha TAKUKURU kuendelea kuaminiwa na wananchi wa taifa la Tanzania.

Kiongozi huyo mkuu wa TAKUKURU amesema nafasi hiyo imetokana na ushirikiano kati ya watumishi pamoja na wanakagera na hatimaye kumfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumuamini na kumteua aongoze TAKUKURU.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!