Header Ads

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB) YAONGEZA SIKU TATU ZA UHAKIKI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajulisha waombaji wote wa mikopo kuwa imeongeza SIKU TATU za kufanya marekebisho kuanzia tarehe 1 hadi 3 Oktoba, 2018.

Waombaji ambao hawajakamilisha maombi yao, kutumia muda ulioongezwa kukamilisha maombi yao kupitia http://olas.heslb.go.tz 
 
Marekebisho yote yafanyike kwa ukamilifu ndani ya mfumo na waombaji hawalazimiki kutuma marekebisho kwa barua pepe au kwa njia ya ‘EMS’.

Kwa maelezo zaidi tupigie kupitia 0736 66 55 33 au 0739 66 55 33 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni.

Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Dar es salaam,
Jumatatu, Oktoba 1, 2018

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!