Header Ads

ZOEZI LA UOKOAJI LAENDELEA JIJINI MWANZA MIILI YA WATU 125 IMEPATIKANA HADI SASA.


ZOEZI LA UOKOAJI LIKIENDELEA KATIKA ZIWA VICTORIA KUFUATIA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV NYERERE.
Na Tunu Herman
Kijukuu Blog Mwanza

MWANZA

 Zoezi la uokoaji wa miili iliyozama katika meli ya Mv. Nyerere ndani ya ziwa Victoria katika kisiwa cha Ukara mkoani  Mwanza bado linaendelea ambapo mpaka sasa miili ya watu zaidi ya 125 imepatikana.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akishilikiana na kamati ya ulinzi na usalamaya mkoa huo na jeshi la wananchi wa TANZANIA, wapigambizi, bado wanaendelea kutafuta miili ya wananchi ambao bado awajapatikana.
Akizungumza katika eneo la tukio Meneja wa Tamesa mkoa wa Mwanza Eng.  Hassan Kalonda amesema meli hiyo iliyozama ilikuwa na wafanyakazi nane (8) ambapo kati ya hao watatu wameokolewa wakiwa wazima huku watano (5)  wanahofiwa kufariki kutokana na miiliyao kutopatikana 
Akiwataja kwa majina wafanyakazi hao ambao miili yao aijapatikana ni Abel Mahatane Nahodha, Agustino Cherehani Fundi, Emmanuel Shinga Karani, Blastus Bundala Mkuu wa Feri na Mathias Thomas Mlinzi.
Kwa upande wake Waziri wa uchukuzi ujenzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema taratibu za kimila na zakidini zitafuatwa katika kuwasitiri waliofariki huku akiwataka wananchi kuendelea kuja kutambua miili ya ndugu zako. 
Aidha ameongeza kuwa  msiba huu ni wa kitaifa hivyo viongozi mbali mbali wameendelea kuwasili na kuongeza nguvu katika kusaidia uokoaji ambapo  Waziri mwenye dhaman ya kamati ya Maafa  Mhe. Jenista Muhagama amekwisha kuwasili.
Naye Kamanda wa polisi nchini Simoni Sirro amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu katika shughuli zinazoendelea za uokoaji na amewataka kutojaribu kufanya matukio yakihalifu kwani jeshi la polisi limejipanda na linahakikisha ulinzi unaimarika muda wote.
Miili yote ya wananchi iliyookolewa imehifadhiwa katika kituo cha afya Bwisya kisiwa cha Ukara. Na zoezi la uokoaji linaendelea.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!