Header Ads

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WAWAPO KAZINI.

KATIBU MTENDAJI WA TUME YA TAIFA YA UNESCO DR MOSHI KIMIZI AKISISITIZA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI)

MWANZA
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuyatambua vyema mazingira wanayofanyia kazi ili kujilinda na hatari zinazoweza kuwakuta wakiwa kazini.

Wito huo umetolewa leo jijini Mwanza na kaimu katibu tawala Mkoa wa Mwanza Warioba Sanya kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo John Mongela wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari yanayoratibiwa na shirika la UNESCO.

Sanya amesema kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira magumu hali inayohatarisha usalama wao na kwamba kutambua mazingira wanayofanyia kazi itawasaidia kujilinda na kuwa salama katika majukumu yao.

Katika hatua nyingine Sanya ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuweka mazingira rafiki kwa waandishi wao ikiwa ni pamoja na swala la uhakika wa usafiri na usalama sehemu za kazi.

Awali akielelzea malengo ya mafunzo hayo katibu mtendaji wa wa tume ya Taifa ya UNESCO Moshi Kimizi amesema kuwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari waweze kujilinda na kutambua hatari zinazowazunguka ili wawe salama katika majukumu yao.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Tabora,Geita,Simiyu,Mara na Kagera ambapo yataendelea tena katika mikoa ya nyanda za kati.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!