Header Ads

SERIKALI MKOANI KATAVI YAONYESHA IMANI KUBWA KWA MSAMBAZAJI WA MBOLEA ZA YARA OBO INVESTMENT.

 
 KATIBU TAWALA WA MKOA WA KATAVI CRESENCIA JOSEPH AKIPATA MAELEKEZO KUTOKA KWA VIONGOZI WA YARA NA OBO INVESTIMENT.

KATAVI
Uongozi wa mkoa wa Katavi umesema utahakikisha changamoto za ucheleweshaji wa mbolea za kupandia na kukuzia kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018-2019 zinaisha kwa kuwasimamia mawakala kutoka kampuni ya Yara kupitia kwa wakala wake mkuu Obo investment ili kufanikisha kupatikana kwa mbolea mapema kabla ya msimu wa kilimo haujaanza na kuleta usumbufu kwa wakulima wa mkoa huo.
                 
Hayo yamezungumzwa na Kaimu katibu tawala mkoa wa Katavi CRESENCIA JOSEPH mara baada ya kuzindua ghala kubwa la kuhifadhia mbolea na kufungua mafunzo elekezi ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima na maafisa kilimo wa kata na vijiji katika mkoa wa katavi.

Akizungumza katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Obo investment Olais Oleseenga amesema wameamua kuweka Ghala kubwa mkoani katavi ili kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.

Olais amesema OBO Investment ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya YARA watahakikisha mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa walipo wahitaji na watahakikisha bei za mbolea zitakua ndogo kwa mkulima mala baada ya kuanza kutumia usafiri treni kutoa mbolea kutoka Dar es salaam mpaka Mpanda katavi.

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Katavi wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao 100 katika wilaya 3 ambao watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo wa Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.

Naye Afisa Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini John Meshak amesema wameamua kuzindua ghala la mbolea Mpanda kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza kasi ya uzalishaji wa mazao yao.

Kwa niaba ya wakulima wa mkoa wa katavi akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake ameipongeza kampuni ya OBO Investment ambao ni wakala mkuu wa YARA kwa kuwafikishia pembeo kwa wakati,na kuongeza kuwa kuanzia msimu ujao uzalishaji utaongezeka kwa kuwa wakulima wamelima na kuwekea mbolea kwa wakati tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa wito kuhakikisha kwamba Mbolea na pembejeo zingine zinapatikana muda wote zinapohitajika tena na kwa gharama nafuu ambapo Kampuni ya OBO Investment ambao ni wakala wakuu wa Kampuni ya Mbolea ya YARA wameanza kutekeleza agizo hilo kwa mikoa ya Mbeya,Songwe, Rukwa, na Katavi.


MATUKIO KATIKA PICHA:VIONGOZI WA DINI,WAKULIMA NA WATUMISHI WAKIWA KATIKA MAFUNZO YA MATUMIZI BORA YA MBOLEA ZA YARA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!