Header Ads

MISINGI YA KUMLEA MTOTO WA KIUME


Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kuzingatia hasa pale unapomlea mwanao wa kiume.

Mpe Majukumu
Kufuata maelekezo na kumaliza kazi wanazopewa wavulana hii kitu huwa ni changamoto sana kuizoea. kwa hiyo akishaanza kukua mzoeshe kumpa vikazi vidogo vidogo ambavyo anaweza kufanya ili aanze kuzoea mapema kufanya kazi mbalimbali na kuzimaliza kama ulivyomuelekeza.

Kama unapika mwambie akuletee ungo, au mwiko hivi vikazi nahisi utakua unavijua, ila kama ulikua hujui hivi vikazi vinasaidia sana mtoto kujifunza namna ya kufanya kazi, kwa hiyo usione kama unamsumbua maana wazazi wa siku hizi kwa upendo tunaongoza.

Muache Akuonyeshe Hisia Zake
Hata kama ni nyakati za furaha wavulana huwa hawaonyeshi ile furaha mpaka mwisho huwa wanafanya kimya kimya moyoni au mpaka awe peke yake, tofauti na wasichana ambao wanaweza furahia na kuruka ruka hapo sebuleni mpaka jikoni bila shida. Mfundishe kijana wako wa kiume kuonyesha hisia zake kama kakasirika muache aonyeshe kuwa amenuna ili mradi awe mstaarabu tu asiwe anavunja vitu.

Usijali Kama Haonyeshi Tabia za Kiume Wakati Mdogo
Kama mtoto wako bado ni mdogo na bado anapenda kuchezea midoli muache aendelee, au ameshaanza kwenda shule na bado unamuona anachezea midoli au anapenda sana katuni, hiyo sio kwamba ni wa ajabu ila ndio umri wake wa kukua kwa hiyoo usidhanie bado ana matatizo fulani.

Mtafutie michezo zaidi ya watoto wa kiume vigari,baiskeli,mpira wa soka.

Msaidie Kutengeneza Marafiki na Mambo ya Kijamii
Wavulana wengi mara nyingi huwa ni wagumu kutengeneza urafiki na mtu kuliko wasichana. wanaweza kucheza kwenye kikundi baada ya hapo yuko kivyake, kwa hiyo hapo anahitaji msaada wako ukiona hivyo kwa kumuunganisha na mtoto mwingine ili atengeneze urafiki wa karibu na watu mbalimbali na umwambie wacheze wote hata kutumia vigari vyake.

Jishirikishe Kwenye Mambo Yake ya Shule
Nenda shule kaongee na walimu wanaomfundisha mtoto wako ili ujue anavyoendelea, madhaifu yake na maeneo anayofanya vizuri. Kisha mwambie kuwa umeonana na mwalimu wake na umeona mapungufu gani kwake na umuulize ni wapi anataka umsaidie zaidi ili afanye vizuri. Angalia homework zake na kumsisitiza angalau ajaribu kumaliza homework zake mapema.

Mpongeze Kwa Tabia Zake Nzuri
Tabia za watoto wa kiume muda mwingine zinachanganya sana wazazi mpaka wakati mwingine unawaza ni jinsi gani ya kumlea mtoto, ila sasa kama ukiona amefanya kitu kizuri au ameonyesha tabia nzuri basi hapo hapo mpongeze na kumjulisha kuwa umependa kitu alichokifanya na umekubali. Ukifanya hivyo unamuongezea hamu ya kuendelea kufanya mambo mazuri kwenye maisha yake.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!