Header Ads

LOWASSA ATUMA SALAMU ZA POLE AJALI YA MV NYERERE

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kutokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere, kilichozama jana Ukerewe, jijini Mwanza.

Ajali hiyo ilitokea jana wakati kivuko hicho kikitoka Bugorora (Ukerewe) kwenda Bwisya (Ukara) kikiwa na abiria wengi ambapo hadi sasa watu zaidi ya 100 wanahofiwa kufariki dunia katika ajali hiyo.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea jana Septemba 20, huko Ukerewe mkoani Mwanza.

“Nawapa pole ndugu wa wote waliopoteza maisha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na watanzania wote kwa ujumla,” amesema Lowassa.

Lowassa amesema huo ni msiba wa nchi nzima kwani maisha ya wananchi wengi namna hiyo yanapopotea kwa ajali, ni lazima tujiulize na kujipanga kama taifa ili yasitokee tena.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!