Header Ads

KAMISHNA WA TRA APATA AJALI DODOMA

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere amepata ajali leo Jumanne, Septemba 11, 2018 baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8 namba STL 5199 kugongana na gari dogo la mtu binafsi lenye namba za usajili T 416 BTH, eneo la Nanenane, jijini Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema, ajali hiyo imetokea na kwamba hakuna madhara kwa binadamu bali ni uharibifu wa magari ndio umetokea.

Gari la Mamlaka ya Mapato lilikuwa likitokea Morogoro kuelekea Dodoma ndipo lilipogongana na gari lililokuwa likielekea chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambalo lilichomoza wakati gari la Kamishna likipita gari jingine.

Amesema gari la Kamishna lilikuwa likiendeshwa na Peter (35) kabila ni Msukuma ambaye ni mkazi wa Kurasini Dar es salaam huku lile jingine lilikuwa linaendeshwa na Paul (39) kabila ni Masai ambaye ni mhadhili wa Chuo Kikuu cha UDOM.

Ameweka wazi kuwa wamejiridhisha mpaka sasa kiafya wahusika wote wako salama.

 

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!