Header Ads

GARI YA WATALII YAPATA AJALI MBAYA JIJINI ARUSHA

Gari ya watalii imepata ajali mbaya  Jijini Arusha.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari  iliyohusisha Lori na gari ya kubeba watalii.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mti mmoja Wilayani Monduli.

Kamanda Ng’anzi amesema gari aina ya Land Cruiser iliyokuwa imebeba watalii imegongana uso kwa uso na Lori la mizigo takribani Kilometa 10 kutoka njia panda ya Monduli.

”Nipo eneo la ajali hapa muda huu, tunaendelea na vipimo hapa, nitawajulisha kwa undani lakini vifo vipo ila bado hatujajua ni idadi gani”, amesema.

Taarifa za awali zinaeleza takribani watu watano wamefariki katika ajali hiyo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!