Header Ads

DC KAHAMA APIGA MARUFUKU LADIES FREE KWENYE MATAMASHA YA STAREHE.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA ANAMRINGI MACHA

KAHAMA
Serikali wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imepiga marufuku matangazo burudani yenye jumbe zinazowanyanyapaa wanawake kwenye matamasha ya muziki na kumbi za disco hasa yenye kusema kiingilio wanawake bure.

Agizo hilo limetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akifungua mafunzo kwa watumishi wa halmashauri ya mjiwa Kahama  pamoja na madiwani na wananchi yanayoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC).

Macha amesema wapo baadhi ya wamiliki wa kumbi za starehe ambao wanatengeneza matangazo ambayo hayatakiwi kusikika kwenye jamii kwani  yanawanyanyapaa wanawake  na kuhamasisha kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kuongeza kuwa atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katika hatua nyingine Macha amewataka wasichana wadogo kuacha tama mabazo zinasababisha kupata VVU na badala yake wajitambue na waachane na makundi yasiyofaa yanayoweza kuwapotezea malengo yao.

Naye mwakilishi wa mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu(LHRC) Felister Mauya amesema dhima kuu ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi wa serikali  na jamiiili kutambua umuhimu wa haki za binadamu hapa nchini.

Akijibu hoja kuhusu upungufu wa zahanti na vituo vya Afya vya kutolea Elimu ya Ukimwi ,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kuongeza kuwa kila mwaka wa fedha halmashauri imejipanga kujenga zahanati na vituo vya afya vitano ili kurahisisha upatikanaji  wa huduma za afya.

MATUKIO KATIKA PICHA:

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ANDERSON MSUMBA AKIZUNGUMZIA UHABA WA ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA KATIKA HALMASHAURI HIYO NA KUELEZA MIKAKATI WALIYONAYO.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABEL SHIJA AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MADIWANI KATIKA MAFUNZO HAYO.

BAADHI YA WANACHI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAKIWA KATIKA MAFUNZO HAYO.


WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAKIWA KATIKA MAFUNZO HAYO

AFISA MIRADI JINSIA NA WATOTO KUTOKA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU GETRUDE DYABENE AKIZUNGUMZA JAMBO KATIKA MAFUNZO HAYO.

BAADHI YA WANANCHI NA VIKUNDI VYA KINA MAMA NA WASICHANA WAKIWA KATIKA MAFUNZO HAYO.

MAFUNZO YAKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA PINE LIDGE MJINI KAHAMA


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!