Header Ads

AKUTWA NA KICHWA CHA BINADAMU KWENYE UVUNGU WA KITANDA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu wawili akiwamo mwenye umri wa miaka 65 kwa tuhuma za kukutwa na kichwa cha binadamu nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla akizungumza mjini Chato leo, alisema waliokamatwa ni mkazi wa kijiji cha Ibondo B na mkazi wa Mwabasabhi wilayani Chato.

Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 8, 2018 ambapo watuhumiwa hao walikua wamekificha kichwa hicho uvunguni mwa kitanda nyumbani kwa mmoja wao.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!