Header Ads

ZIMA MOTO KAHAMA YAWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MAJANGA YA MOTO MAPEMA KABLA YA KUANZA KUZIMA KWA NDOO.


ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO KAHAMA WAKISAIDIANA NA WANANCHI KUUDHIBITI MOTO ULIOKUWA UNATEKETEZA NYUMBA YA BWANA IDDI MASOME MAARUFU MURAAA ILIYOPO ENEO LA NYAKATO PHAMTOM KAHAMA.

KAHAMA
WANANCHI Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutoa taarifa za majanga ya moto mapema yanapotokea na kuacha tabia ya kuanza kuuzima kwa vitendea kazi duni na wanapozidiwa ndipo wanapiga simu kituo cha zima moto na Uokoaji.

Wito huo umetolewa leo na Afisa wa jeshi la zima Moto na Uokoaji Wilayani Kahama, FRANK ELOPHAZY wakati wa zoezi la uokoaji wa nyumba ya Bwana IDDI MASOME iliyoteketezwa kwa moto leo mchana majira ya saa 7 mchana mtaa wa Nyakato, mjini Kahama.

Sambamba na hayo, ELOPHAZY amewataka wananchi kuacha kuweka ndani vitu vinavyochagiza moto kama ilivyokuwa kwa nyumba ya MASOME ambayo ilikuwa na magodoro mengi na mbao zilizokuwa katika dari, hali ambayo imesababisha moto kuwa mkubwa na kushindwa kuokoa mali zozote.

Pamoja na hayo ELOPHAZY amewataka wananchi kuacha kuvichezea visima vya maji ya dharula(FIRE HYDRANT) vilivyopo katika mitaa yao kwani visima hivyo vinasaidia katika uokoaji wakati ambapo gari linaishiwa maji kama kilivyosaidia kuuzima moto wa nyumba hiyo. 

Kwa upande wake mmiliki wa Nyumba hiyo Bwana Iddi Masome amesema kuwa amepata taarifa akiwa kazini na nyumbani aliwaacha watoto wake wawili na kwamba amepata hasara ya kuunguliwa vitu vyote  vilivyokuwa ndani.

Naye Bwana Emmanuel Daudi  ambaye ndiye aliyetoa taarifa kwa mwenye nyumba  amesema kuwa yeye alikuwa alikuwa anapita njiani na ndipo alipoona moshi unatoka na ndipo alipoomba msaada kwa wapiti njia kusaidia kuuzima moto huo kabla ya kupiga simu kikosi cha zima moto.

Naye mtoto wa mmiliki wa Nyumba hiyo Clencia Masome amesema kuwa yeye alikuwa nje anafua na mdogo wake alikuwa ndani,ndipo alipoona moshi na kuamua kuzima kwenye Mita ya umeme ilishindikana akaona atoe taarifa kwa majirani.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa jeshi la zima moto chanzo cha moto huo ni Hililafu ya umeme na kwamba tathimini inafanyika kujua hasara iliyotokea kutokana na moto huo. 

 MATUKIO KATIKA PICHA:
 
 WANANCHI WA MJINI KAHAMA WAKISAIDIANA NA ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO KUHAMISHA MPIRA WA MAJI ILI KUENDELEA KUUZIMA MOTO HUO.


ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKIENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUUDHIBITI MOTO KATIKA ENEO LA NYAKATO.
HIVI NDIVYO NAMNA NYUMBA ILIVYOKUWA INATEKETEA KATIKA ENEO LA NYAKATO.

HALI ILIVYOKUWA KATIKA ENEO HILO HAPA WANANCHI NA ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKIENDELEA KUUDHIBITI MOTO.

ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WAKISAIDIANA NA WANANCHI PAMOJA NA MADEREVA BODA BODA KUZIMA MOTO.
HALI ILIVYOKUWA KATIKA MOJA YA CHUMBA AMBACHO KILIKUWA NA MAGODORO MENGI NA MILANGO PAMJA NA MABAO.

MOJA YA CHUMBA AMBACHO KILIKUWA NA MAGODORO NA TV,KIKIWA KATIKA HALI MBAYA MARA BAADA YA ASKARI WA ZIMA MOTO KUWEKA JUHUDI ZA KUUZIMA MOTO.

KAMANDA WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO WILAYANI KAHAMA FRANK AKIANGALIA ZOEZI LA UZIMAJI MOTO LIKIENDELEA.

WANANCHI WAKISHIRIKIANA NA ASKARI WA KIKOSI CHA ZIMA MOTO KUHAKIKISHA ZOEZI LINAENDA SALAMA KATIKA KUUZIMA MOTO HUO.

MMILIKI WA NYUMBA ILIYOUNGUA BWANA IDDI MASOME .

GARI LA ZIMA MOTO LIKIWA ENEO LA TUKIO KATIKA HARAKATI ZA KUUDHIBITI MOTO.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!