Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WANANCHI MSALALA KAHAMA HAWAJUI WAPO KATIKA KATA GANI KUFUATIA MGOGORO WA MPAKA.


MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MSALALA SAIMON BEREGE.

KAHAMA
Halimashauri ya Msalala wilayani Kahama imeshauriwa kutatua mgogoro wa wananchi wa kata ya Mega na  Segese kuhusu mpaka wa kijiji cha Masabi kutokana na mgogoro huo kuzidi kuwa mkubwa na  hivyo kusababisha  hofu ya usalama wa maisha yao.

Akizungumza jana  katika kijiji cha Ntobo kwenye Kikao cha baraza la madiwani diwani wa Kata ya Mega Patrick Mazuli amesema  mbali na hofu hiyo pia mgogoro huo unarudisha nyuma Maendeleo ya wananchi waliopo mpakani hapo kwani hawajui kata inayowahudumia.

Amewaomba wakuu wa idara ya ardhi kwenda kuzungumza na wananchi pamoja na kuweka mipaka haraka ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mgogoro huo.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mibako Mabubu ameitaka halmashauri hiyo kulipatia ufumbuzi suala hilo ili lisilete madhara makubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake kaimu Afisa ardhi na maliasili halmashauri hiyo Lazaro Ndenga amesema wanakusudia kujenga mpaka unaoonekana katika mpaka huo huku Mkurugenzi mtendaji wa halmashaur hiyo  Simon Berege akisema atatuma wataalam haraka iwezekenavyo ili wakaongee na wananchi wa maeneo hayo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News