Header Ads

WAJAWAZITO KAHAMA WATAKIWA KUACHA TABIA YA KWENDA KLINIKI NA WANAUME FEKI.

 MRATIBU WA KUDHIBITI UKIMWI HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA DKT HERRY SYLIVESTER AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA KARTAS MJINI KAHAMA.

KAHAMA
Kina mama wajawazito wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha tabia ya kwenda Kliniki na wanaume wasiyo waume zao ili kupewa kipaumbele katika huduma ya upimaji wa virusi vya ukimwi badala yake waende na waume zao halali waliowapa ujauzito.

Wito huo umetolewa leo na mratibu wa Kudhibiti ukimwi halmashauri ya mji wa Kahama Dkt Herry Sylivester katika mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu ukimwi na haki za binadamu yanayoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC).

Sylivester amesema kuwa kina mama wanaofanya hivyo wanajidanganya wenyewe na kwamba maambukizi waliyonayo waume zao yataendelea kuwepo na wao kuwa katika hali ya hatari ya kuambukizwa.

Katika hatua nyingine Sylvester ametoa wito kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza virusi hivyo pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu ili kuwa na afya njema.

Wakielezea sababu zinazowafanya kina mama wajawazito kutokwenda na waume zao halali baadhi ya waandishi wa habari wamesema kuwa inatokana na wengi wao kupewa ujauzito na wanaume wa watu pamoja na uwoga wa wanaume hao kwenda kupima ukimwi.

Awali akifungua mafunzo hayo afisa utawala wa kituo cha Sheria na haki za binadamu Theresia Kinabo amesema kuwa kundi la waandishi wa habari ni muhimu katika jamii na kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kutoa taarifa sahihi kuhusu masuala ya Ukimwi na haki za binadamu.

Kwa upande wake Afisa Miradi jinsia na watoto kutoka kituo cha sheria na haki za Binadamu Getrude Dyabene amewataka waandishi wa habari kuzingatia weledi na maadili katika majukumu yao hususan katika  kuandika habari zinazohusu watoto ili kulinda utu wao.


Kituo cha Sheria na haki za binadamu(LHRC) kinatoa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi habari 20 kutoka vyombo mbalimbali vya habari Wilayani Kahama kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya Ukimwi na haki za binadamu.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 AFISA UTAWALA WA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU BI THERESIA KINABO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WILAYANI KAHAMA.


 AFISA MIRADI JINSIA NA WATOTO KUTOKA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU GETRUDE DYABENE AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI KATIKA MAJUKUMU YAO.

 AFISA MIRADI JINSIA NA WATOTO (KULIA) GETRUDE DYABENE AKIWA NA AFISA UTAWALA WA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BIANDAMU WAKILI THERESIA KINABO WAKIFUATILIA DARASA WAKATI MRATIBU WA KUDHIBITI UKIMWI DR HERRY SYLIVESTER AKIENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UKIMWI( HAYUPO PICHANI)

 WAANDISHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI WILAYANI KAHAMA WAKIWA MAKINI KUFUATILIA SOMO LA HAKI ZA BINADAMU KUTOKA KWA WAKILI THERESIA KINABO.


 KUTOKA KUSHOTO NI SHABANI NJIA WA GAZETI LA NIPASHE,KATIKATI NI NEEMA MGHEN KUTOKA KAHAMA FM NA KUSHOTO NI PAULINA JUMA KUTOKA KAHAMA FM.
 WAANDISHI WA HABARI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU,KUTOKA KUSHOTO MARCO MIPAWA,KATIKATI NI RAYMOND MIHAYO NA KULIA NI ALLY LYTAWI.

 WAANDISHI WA HABARI WAKIENDELEA KUPATA MAFUNZO KATIKA UKUMBI WA KARTAS MJINI KAHAMA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!