Header Ads

WAGONJWA KAHAMA WAHOFIA KUPONDWA NA JENGO LA ZAHANATI.


DIWANI WA KATA YA KINAMAPULA SHARIF SAMWELI AKIONGEA KUHUSU UBOVU WA JENGO HILO KATIKA  BARAZA LA KAWAIDA LA MADIWANI HALMASHAURI YA USHETU.

KAHAMA
Wananchi wa kata ya Kinamapula halmashauri ya ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba Serikali kufanya marekebisho ya jengo la Zahanati ya kata yao ambalo limeweka nyufa hali inayotishia usalama wa mama wajawazito na wagonjwa wengine.

Akiongea kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani  kwa niaba ya wananchi,diwani wa kata ya Kinamapula Sharif Samweli amesema kuwa jengo hilo linavuja na ameshatoa taarifa  siku nyingi na kwamba kwa sasa hali ni mbaya kwani matofai yanadondoka.

Katika hatua nyingine Samweli ameongeza kuwa kama ukarabati wa jengo hilo hautofanyika kwa sasa ni bora huduma za afya zisitishwe kwa muda kuliko kuja kupata tatizo la mgonjwa kupondwa na tofali na kukatisha maisha yake.

Akijibu swala hilo Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomola amesema kuwa jengo hilo Halikujengwa kwa ubora na wananchi na kwamba halmashauri ina mpango wa kuliezua na kulirekebisha upya kwa kuliiinua juu zaidi.

Zahanati ya Kata ya Kinamapula imejengwa mwaka na inahudumia wananchi wanaokadiliwa kufikia 700 kutoka vijiji 6 vyenye vitongoji 36.No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!