Header Ads

LHRC YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KAHAMA,KUZINGATIA SHERIA NA MAADILI KATIKA KAZI ZAO.


 AFISA MAWASILIANO KUTOKA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU MICHAEL MALLYA
 KAHAMA
Waandishi wa habari wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya kazi  kwa kufuata maadili na sheria ili kuwa huru katika majukumu yao na kupunguza madhara kwenye jamii.

Wito huo umetolewa leo na afisa mawaAsiliano kutoka kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) Michael Mallya katika mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuangazia Haki za binadamu na uandishi wa habari za ukimwi.

Mallya amesema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia maadili  ya jamii wanazotoka ili waandike habari zinazoweza kuisaidia jamii husika kuondokana na imani potofu zinazosababisha madhara.

Katika hatua nyingine Mallya amewataka waandishi wa habari kutafuta taarifa sahihi kabla ya kuandika habari zao ili kutochochea migogoro katika jamii.

Sambamba na hayo Mallya amewaonya waandishi wa habari kuacha  kupokea rushwa na kwamba vitendo hivyo vinasababisha kuficha ukweli na kuuonea upande mwingine ambao haukutoa rushwa.

Kwa upande wao baadhi ya waandishi wa habari wilayani Kahama wamekishukuru kituo cha sheria na haki za binadamu kwa kuwapatia mafunzo hayo na kwamba imewasaidia kujua mambo mengi ya kimaadili na sheria ambayo walikuwa hawayafahamu.

Kituo cha sheria na haki za binadamu kimetoa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari 20 wa wilayani Kahama kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari wilayani humo.


MATUKIO KATIKA PICHA;

 WAANDISHI WA HABARI KUTOKA RADIO DIVENE YA MJINI KAHAMA WAKIWA KATIKA MAFUNZO,KUTOKA KUSHOTO NI THEONESTINA GREGORY NA TSUMAI SALUMU

 KUTOKA KUSHOTO PAUL KAYANDA WA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA,SEBASTIAN MNAKAYA WA RADIO KAHAMA,NYAMITI ALPHONCE WA DIVINE FM NA PATRICK MABULA WA GAZETI LA MAJIRA.

 WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA MAFUNZO KATIKA UKUMBI WA KARTAS MJINI KAHAMA.

 MWANDISHI WA GAZETI LA MWANANCHI SHIJA FELICIAN KUSHOTO AKIWA NA NEEMA SAWAKA KATIKATI WA GAZETI LA NIPASHE NA NEEMA MGHEN WA KAHAMA FM.

 MWANDISHI WA HABARI WA RADIO KWIZERA WILAYANI KAHAMA SAIMON DIONIZ AKIWASILISHA KAZI YA KIKUNDI KUHUSU MAMBO YA KUEPUKA KATIKA KURIPOTI HABARI ZA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI.

 WAANDISHI WA HABARI WAKIWA DARASANI WAKIENDELEA KUPATA MAFUNZO.

 MWANDISHI WA HABARI KUTOKA RADIO DIVINE FM THEONESTINA GREGORY AKIWASILISHA KAZI YA KIKUNDI KUHUSU KAZI ZA WAANDISHI WA HABARI KATIKA JAMII.

 KUTOKA KUSHOTO MARCO MIPAWA WA KAHAMA FM,KATIKATI NI RAYMOND MIHAYO WA GAZETI LA TANZANITE NA ALLY LYATAWI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA WAKIWA DARASANI KATIKA MAFUNZO HAYO.

 WAANDISHI WA HABARI WAKIWA DARASANI WAKIENDELEA NA MAFUNZO KATIKA UKUMBI WA KARTAS MJINI KAHAMA.

 KUTOKA RADIO HUHESO FM ANAITWA JUMA MWESIGWA AKIWASILISHA KAZI YA KIKUNDI KUHUSU UMUHIMU WA VYOMO VYA HABARI KATIKA JAMII.

 PASCHAL MALULU MWANDISHI WA GAZETI LA MTANZANIA AKIWASILISHA KAZI YA KIKUNDI KUHUSU UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI.

 WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA KAZI ZA VIKUNDI

WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA KAZI ZA VIKUNDI.
No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!