Header Ads

WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA AWAAGIZA WANANCHI KUZIFUATA DAWA ZINAZOIBIWA NA WAHUDUMU WA AFYA.

Na, Magdalena Kashindye
Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kasim Majaliwa amewaagiza wananchi kuzilinda dawa katika hospital zote nchi.

Majaliwa amesema hayo wakati akihutubia wanchi wa halmashauri ya Ushetu iliyopo wilayani Kahama mkoani shinyanga katika uzinduzi wa bima ya Afya kwa wakulima wa vyama vya msingi.

Waziri Majaliwa amewaambia wananchi pindi watakapowaona wahudumu wa Afya wanaiba dawa ni vema wakawatarifu viongozi ili waandamane nao kuzifuata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Majaliwa amezindua Mradi wa bima ya Afya kwa wakulima wa vyama vya msingi, bima hizo zitawawezesha kutibiwa bure popote nchini

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!