Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WAZIRI WA KILIMO MH TIZEBA AFUNGUA MASOKO YA TUMBAKU KITAIFA MJINI KAHAMA,ATOA ONYO KWA WAKULIMA WANAOLIMA ZAO HILO NJE YA MFUMO.

  Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikata utepe kuashiria ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa katika sherehe iliyofanyika kwenye viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.

 KAHAMA
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba Leo amefungua masoko ya tumbaku Kitaifa huku akitoa onyo kali kwa wakulima waliolima zao hilo nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu wa sheria ya zao hilo kwa kuwataka kuacha mara moja kwani serikali itashughulika na wote wanaokiuka taratibu za kilimo hicho.

Dkt Tizeba ameyasema hayo leo 12 Juni 2018 katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati akihutubia mamia ya wakulima wa tumbaku kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa.

Dkt Tizeba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack kufanya kikao na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa huo kuhakikisha wanazuia wananchi kulima nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu ya sheria ya zao la tumbaku.

Alisema kuwa wigo wa soko la tumbaku unazidi kuwa finyu kutokana na viongozi mbalimbali kuwakumbatia baadhi ya wakulima wa tumbaku wanaolima nje ya mfumo wa zao hilo.

Katika sherehe hiyo Mhe Dkt. Tizeba amekabidhi vyeti vya pongezi kwa wakulima waliofanya vizuri katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 ambao ni mkulima Emmanuel Cherehani kutoka Wilaya ya Ushetu aliyeshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ni Jimson Mwanjwenga kutoka Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wakulima wa zao la tumbaku Tanzania Kaimu Meneja Mkuu TCJE Ndg Bakari Kisia alisema kuwa zao la tumbaku limeanza kulimwa nchini Tanzania enzi za ukoloni kwa kuanzia mikoa ya Ruvuma (Tumbaku ya Moshi) na Iringa (Tumbaku ya mvuke) huku akisema kuwa umaarufu wa zao hilo umekuja mara baada ya masoko huria kuanzishwa.

Kisia amepongeza juhudi za serikali katika misimu miwili ya mwaka 2016/2017 na 2017/2018 kwa kutatua suala la kupanda kwa bei ya pembejeo huku akizitaja changamoto katika zao la tumbaku kuwa ni pamoja na kupungua kwa mahitaji ya tumbaku, Kushuka kwa bei ya wastani ya tumbaku, pamoja na Ukubwa wa riba za mikopo.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya zao la tumbaku Tanzania Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya tumbaku Tanzania Dkt Julius Ningu ameitaja mikoa inayolima tumbaku kwa wingi kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya, Morogoro, Iringa, Ruvuma na Mara huku akiutaja mkoa wa Tabora kuongoza kwa uzalishaji kwa takribani asilimia 50 ya tumbaku yote inayozalishwa nchini.

Alisema kuwa zao la tumbaku lina mchango mkubwa katika pato la Taifa ambapo pato la mkulima limeongezeka kutoka shilingi za kitanzania 2,242,030 mwaka 2011/2012 hadi shilingi 5,982,745 mwaka 2016/2017 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 166.8.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa wakulima wa Tumbaku Tanzania (TCJE) ambaye  pia ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha wakulima Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani ameiomba Serikali kurejesha ununuzi wa zao la Tumbaku kwa bei ya Dola kwani kununua kwa Shillingi ya Tanzania inawaumiza Wakulima.
Akijibu Ombi hilo waziri Tizeba amesema kuwa dola haiwezi kurejeshwa na badala yake siku ya soko linapofanyika wanunuzi na wakulima waangalie kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kwa siku hiyo na ndipo bei hiyo iandikwe

Naye Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandika  anayetoka katika jimbo wanalolima Tumbaku ameipongeza wizara ya Kilimo kwa kusimamia bei na kusimamia mazao vizuri na kuongeza kuwa Wizara yake itaboresha miundo mbinu ya barabara nchi nzima ili kuhakikisha wakulima wanafikiwa na huduma nzuri za barabara.

Makusanyo ya ushuru wa Halmashauri za Wilaya yameongezeka kutoka shilingi bilioni 10.8 mwaka 2011/2012 hadi shilingi bilioni 14.8 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 37. Huku mapato ya fedha za kigeni yakiwa yameongezeka kutoka dola milioni 302.8 mwaka 2011 hadi dola milioni 343.9 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 14.
MATUKIO KATIKA PICHA:
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.  
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akimkabidhi cheti cha pongezi Mkulima Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ambaye ameshika nafasi ya tatu katika msimu wa kilimo cha tumbaku wa mwaka 2017/2018 wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.

 Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani akipokea Cheti na zawadi ya Mshindi wa Kanza wa Mkulima Bora wa Tumbaku.
Waziri wa kilimo ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Masoko ya Tumbaku Dkt Charles Tizeba akimpa Pongezi mkulima bora wa zao la Tumbaku Emmanuel Cherehani ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha wakulima Kahama (KACU)  

 Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akimkabidhi cheti cha pongezi Mkulima Jimson Mwanjwenga kutoka mbeya aliyeshika nafasi ya Pili kwa Ukulima Bora Nchini.

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akishuhudia ununuzi wa tumbaku wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Baadhi ya wakulima wa tumbaku wakishuhudia sherehe za uzinduzi wa ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Dr Julius Ningu Kushoto akisoma taarifa ya Zao la Tumbaku mbele ya Mgeni Rasmi,Kulia ni Mmiliki wa Blog Hii William Bundala ambaye alikuwa Mc wa Ghafla Hiyo.


Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu Akitoa neno Kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkao wa Shinyanga Bi Zainab Tellack kutoa neno.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
 
Kaimu Meneja Mkuu TCJE Ndg Bakari Kisia akisom Risala kwa niaba ya wakulima wote nchini.

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akiwa na Baadhi ya viongozi wakielekea Kwenye eneo la Tukio kwa ajili ya Ufunguzi Rasmi wa Masoko ya Tumbaku.


Viongozi wa vyama vya msingi kutoka vyama vya Msingi vya Tumbaku wakiwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa masoko ya Tumbaku.
Baadhi ya wakulima wa zao la Tumbaku walioingiza Tumbaku zao kwa ajili ya Kuuza wakimsikiliza kwa Makini Waziri wa Kilimo Hayupo Pichani.

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza na wakulima nje ya Ghala la Tumbaku,hapa akitolea ufafanuzi kuhusu kununua Tumbaku kwa Bei ya Shillingi na Siyo Fedha za Kigeni.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Dr Julius Ningu aliyeinua Mkono Akitolea ufafanuzi jambo mbele ya Waziri wa Kilimo Mh Tizeba.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News