Header Ads

UKWELI KUHUSU MOTO ULIOWAKA KATIKA OFISI YA RIDHIWANI KIKWETE.

Ofisi ya Mbunge jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete iliyopo eneo la Msolwa, Chalinze imeungua kwa moto jana jioni ya Jumapili, Juni 17, 2018 huku mali, samani na nyaraka zilizokuwemo ndani ya jengo hilo zikitejetea vibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Jonathan Shana amethibitisha na kusema chanzo cha moto huo ni mwanamke anayedaiwa kuwa ana matatizo ya akili ‘kichaa’ alikuwa na moto nje ya ofisi, upepo ulipopiga ulisukuma moto ukashika jengo.

Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio lakini tayari moto ulikuwa umeshashika jengio zima.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!