Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

SERIKALI YAWASHUKIA MAAFISA UTUMISHI WANAOCHELEWESHA MALIPO YA WASTAAFU

Serikali imesema mtumishi wa umma anayestaafu anatakiwa kulipwa mafao yake ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria na kinyume na hapo waajiri watawajibishwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Ijumaa Juni 9, 2018 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika wakati akizungumza na waandishi wa habari, kupiga marufuku wastaafu kufuatilia mafao yao kwa kuwa kazi hiyo inapaswa kufanywa na maofisa utumishi.

Amesema kumekuwa mateso na usumbufu kwa wastaafu ambao wanachukua muda mrefu kulipwa mafao yao licha ya kuwa ni haki yao.

Kauli ya Mkuchika imekuja huku kukiwa na idadi kubwa ya watumishi wanaosotea mafao yao na baadhi wakitumia muda mrefu na wengine kufariki dunia bila kupata fedha hizo.

"Utakuta mtu anaishi Bukoba lakini anafuata haki yake Dar es Salaam na kila siku analala na kula hivyo kujikuta akitumia gharama kubwa ambazo ni mateso kwake, tunasema sasa mambo kama hayo hayapaswi kuwepo tena,” amesema Mkuchika

Amewataka maofisa utumishi wote kutimiza wajibu wao wa kuwasaidia wastaafu kupata haki yao vinginevyo Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali.

Kuhusu hatua za kufuata ili kupata mafao, amesema zinaanzia kwa waajiriwa wenyewe ambao miezi sita kabla wanatakiwa kuandika barua za kueleza mwezi na tarehe za kustaafu kwao kabla ya mwajiri naye kuitaarifu mifuko.

Amesema hatua ya tatu ni kwa mifuko ya pensheni ambayo nayo inatakiwa kuandaa nyaraka muhimu ambazo zitamwezesha mstaafu kupata haki yake mapema.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News