Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MH LEMBELI ARUDI CCM,MAMA YAKE ANENA MAZITO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI.


MAMA MZAZI WA DAUD JAMES LEMBELI,MARIA KASEMBO LEMBELI AKIZUNGUMZA MBELE YA HADHARA KUMTAKA MWANAYE AWEKE WAZI KURUDI CCM

KAHAMA
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kahama Mjini mwaka 2015 kupitia CHADEMA na mbunge wa Jimbo la KAHAMA tangu mwaka 2005 hadi 2015 kupitia CCM, JAMES LEMBELI amejivua uanachama wa CHADEMA na kutangaza rasmi kurejea CCM.

LEMBELI ametangaza uamuzi huo leo katika kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika kijijini kwake Mseki Bulungwa Kahama baada ya Mama yake Mzazi kumtaka kuchukua uamuzi huo kwani hakuridhishwa na uamuzi wake wa kuhamia CHADEMA.

Akitoa salamu za familia, mama mzazi wa LEMBELI, MARIA KASEMBO LEMBELI amesema hakufurahishwa na kitendo cha mtoto wake kuhamia upinzani hali iliyomfanya kwenda JERUSALEM kufanya maombi ili Lembeli arudi CCM.

Pamoja na hayo LEMBELI amemuomba radhi rais Dkt. JOHN POMBE MAUFULI kwa kuchelewa kuitikia wito wake wa kumtaka kurejea CCM ili washirikiane kuijenga nchi alioutoa katika mkutano wake wilayani Kahama mwaka 2016.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kurejea CCM, LEMBELI alitaka kuachana na siasa ili kufanya kazi na  taasisi ambazo zimempa heshima ya kuwa mwakilishi wake nchini ikiwemo Taasisi ya JANE GOODALL ya nchini Marekani ambayo ni mwenywekiti wake.

Katika mkutano huo wanachama wengine 6 ambao waliingia CHADEMA Agosti 21 mwaka 2015 kumfuata LEMBELI, pia wametangaza kurejea CCM.

 MATUKIO KATIKA PICHA:

MH LEMBELI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


MH LEMBELI AKITETA JAMBO NA KAKA YAKE CHIEF PETER LEMBELI,PEMBENI NI MAMA YAO MARIA KASEMBO LEMBELI.

 MH LEMBELI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

 KAKA YAKE NA MH LEMBELI CHIEF PETERLEMBELI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA MAAMUZI YA MDOGO WAKE.

 SHANGWE ZA KUMPONGEZA MH LEMBELI ZIKIENDELEA KATIKA VIWANJA VYA NYUMNBA YAO KIJIJINI MSEKI BULUNGWA.

 WANANCHI WAKIENDELEA KUMPONGEZA MH LEMBELI

WANANCHI NA WAGENI WALIOHUDHURIA TUKIO HILO WAKIMPONGEZA MH LEMBELI KWA MAAMUZI YAKE.

 MH DAUD JAMES LEMBELI AKIWA AMEVAA NGUO ZA KIMILA WAKATI NGOMA YA NYIMBO ZA KIMILA ZIKIPIGWA.

 WAZEE WA KIMILA WAKIPIGA NGOMA YA KIMILA ISHARA YA KUTENDEKA JAMBO ZITO KATIKA FAMILIA YA KITEMI.

 MH DAUD JEMES LEMBELI KUSHOTO AKIWA NA MTANGAZAJI WA KAHAMA FM AMBAYE NI MMILIKI WA KIJUKUU BLOG 

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News