Header Ads

ZITTO KABWE:NIPO TAYARI KUKAMATWA , KUUAWA RIPOTI YA CAG'

Baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey PolePole kusema Zitto Kabwe alidanganya kuhusu Ripoti ya CAG ya upotevu wa TRILIONI 1.5, Zitto amemjibu kwa kuandika yafuatayo;

"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG

"Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni Mia Tano,

"Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa) , Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie"

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!