Header Ads

TFF: KUIONA SIMBA NA YANGA APRIL 29 NI TSH 7000 KWA TSH 30000

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza rasmi viingilio vya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara Aprili 29, 2018 ambao unatarajiwa kuwa kutanisha Simba SC dhidi ya watani wao jadi Yanga utakaopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na uongozi wa TFF na kusema katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika saa 10:00 jioni, kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba (7,000) wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi elfu 30.

"Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi elfu 30, VIP B na C shilingi elfu 20 na upande wa mzunguko kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani itakuwa shilingi elfu saba", imesema taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine, TFF imesema zoezi la upatikanaji tiketi za kuingia uwanjani kwa sasa zipo tayari kupitia mtandao wa selcom.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!