Header Ads

SERIKALI YADAI KUDHARAULIWA..YAWAFUKUZA KAZI WAUGUZI

Serikali imewafukuza kazi wauguzi wote waliokuwa wanashiriki mgomo, baada ya kukataa kurejea kazini licha ya mwajiri wao kuridhia madai yao na kuwaongezea pesa, nchini Zimbabwe.

Katika taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais, Constantino Chiwenga imesema serikali imekerwa na imeona imedharauliwa kwa kiasi cha dola za Marekani 17,114,446 ambazo ni sawa na takribani 39 bilioni za Tanzania, kilichowekwa kwenye akaunti ya Wizara ya Afya ili kushughulikia malalamiko yao.

"Hii ilikuwa ishara ya nia njema ya serikali, uamuzi wa ghafla wa kuhamisha fedha katika mazingira haya magumu ya kiuchumi yanayoikabili nchi hayajaweza, kuwashawishi wauguzi kurejea kazini ili kuokoa maisha ya wagonjwa na kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji msaada wao. Sasa inachukulia kwamba huu ni ukosefu wa huruma kwa vile wanachochewa kisiasa na pia ni kwenda kinyume cha masharti ya kazi na utumishi wa umma" amesema Makamu wa Rais Constantino Chiwenga

Tayari Rais Emmerson Mnangagwa ameidhinisha kufukuzwa kazi na kuhakikisha wauguzi wapya wenye mafunzo wanaajiriwa haraka iwezekanavyo ili waweze kuokoa maisha ya wagonjwa.


Manesi hao waliandamana kudai serikali kuwaongezea mishahara na kuboresha mazingira yao ya kazi, jambo ambalo serikali ya Zimbabwe iliamua kulitatua mara moja.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!