Header Ads

POLISI WAENDELEA KUMSHIKILIA MAMA ALIYEWAWEKEA VYUPA VILIVYOSAGWA KWENYE UJI WATOTO WA MWENYE NYUMBA WAKE KAHAMA.Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mkazi wa Mhongolo mjini Kahama, GRACE KASHINDYE (23) kwa Tuhuma ya kuwawekea vipande vya Chupa vilivyosagwa kwenye uji Watoto wa 5 wa familia moja baada ya wazazi wao kwenda Msibani.

Kamanda wa Polisi mkoani humo SIMON HAULE amesema tukio hilo limetokea Aprili 15 mwaka huu mjini humo ambapo baada ya kubainika kwa tukio hilo watoto hao walipelekwa Polisi na kisha kupelekwa hospitali kwaajili ya uchunguzi. 

Ameyataja majina ya watoto hao kuwa ni EUNICE KULWA (10), AGNES KULWA (7) ALEX KULWA (5) SHADRACK ZENGO (7) na SUZANA ZENGO (3)

Amesema Watoto hao bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hosptali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri ingawa amesema uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea.

Kamanda HAULE amesema chanzo cha tukio hilo bado hakija fahamika na mpaka sasa wanasubiri taarifaa za kitabibu kutoka kwa Madaktari wa hospital hiyo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!