Header Ads

MIILI YA WALIOKUFA 1994 YAGUNDULIWA NA KUZIKWA RWANDA

Maelfu ya watu wamejitokeza katika eneo la Ruhanga kutoa heshima za mwisho na kuzika miili ya watu 150, wahanga wa mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994, yaliyogunduliwa hivi karibuni.

Mazishi hayo yamefanyika katika eneo la makumbusho ya mauaji ya Kimbari la Ruhanga ambalo lipo kariibu na kanisa la Aglikana la Ruhanga, ambalo nalo limetumika kama kaburi la wahanga wa mauaji hayo, ikiwemo miili ya watu zaidi ya  elfu 36 walizikwa ndani ya kanisa hilo.

Kanisa la Ruhanga ni moja ya maeneo ambayo watu wengi waliuawa wakati wa mauaji ya Kimbari, baada ya kukimbilia huko kutafuta salama yao kutoka kwa watu waliokuwa wanaua wenzao.

Mauaji ya Kimbari ni miongoni mwa matukio mabaya kuwahi kuikumba Afrika na dunia kiujumla, ambayo yaliua watu takriban milioni moja huku wengi wao wakiwa wa kabila la Watutsi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!