Header Ads

BAADA YA RC MAKONDA KUJA NA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZEWA WATOTO NA WANAUME,MKUU WA WILAYA YA KAHAMA AJA NA HII.


Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema imebaini kuwa kampuni na mashirika mengi wilayani humo hayatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wake.

Kutokana na hali hiyo, mkuu wa wilaya hiyo, FADHILI NKURLU ameziagiza kampuni na mashirika yaliyomo wilayani humo kuhakikisha wanatoa mikataba ya ajira kwa watumishi wao na kuonya kuchukua hatua za kisheria kwa wote watakaopuuza agizo hilo.

Ameongeza kuwa kuanzia mwezi wa tano atawaita ofisini kwake wafanyakazi wote walioajiliwa kwenye makampuni na sekta mbali mbali ambao hawana mikataba ili kuanza kuwafuatilia waajiri ambao hawatoi mikataba.

Katika hatua nyingine NKURLU amesema Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Shinyanga  utaifunga barabara ya Kahama  - Mwanza kupitia Bulige kutokana na kuharibiwa na mvua kubwa zinazonyesha wilayani humo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!