Header Ads

ASKARI POLISI MWENYE KESI YA RUSHWA AKAMATWA TENA AKIPOKEA RUSHWA

Askari Polisi Mwenye Kesi ya Rushwa Akamatwa Tena Akipokea Rushwa


Askari Polisi mmoja jijini Nairobi ambaye kesi yake ya madai ya rushwa inasikilizwa mahakamani ameshangaza watu baada ya jumatatu April 16, 2018 kukamatwa na polisi kwa kosa la rushwa tena.

Inaripotiwa kuwa askari huyo alikamatwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC) ya nchini humo kwa kuchukua hongo katika uwanja wa mprira wa jiji hilo Nairobi.

Askari huyo Kopro Dan Mburu alikutwa na Shilingi za Kenya 3,250 sawa na Shilingi za Kitanzania 73,450 mifukoni mwake ambazo ndizo alikuwa amepewa kama hongo

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!