Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

BENKI YA CRDB TAWI LA KAHAMA IMETOA HUNDI YA SHILINGI MILIONI NANE KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA ULOWA HALMASHAURI YA USHETU.


KAHAMA
Benki ya CRBD imetoa hundi ya shilingi milioni 8 kwaajili ya ukamilishaji wa Jengo la Zahanati Katika Kijiji cha Kangeme kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
 
Akikabidhi hundi hiyo jana kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Dr Charles Kimei,Meneja wa benki ya CRDB tawi la Kahama, LUTER MNENEY amesema benki hiyo imeamua kutoa mchango huo kwakuwa wakazi wa ulowa ni wadau wa Benki yao kibiashara kupitia zao la Tumbaku.

Sambamba na hayo Mneney ametoa wito kwa Maafisa Ugani na maafisa Ushirika kutoa elimu kwa wakulima wa Tumbaku walime kwa kufuata utaratibu na makisio ya Uzalishaji kwani zao la tumbaku ni zao la mkataba na Sheria.

Awali akisoma risala ya Zahanati hiyo Mganga mfawidhi wa Zahanati Doctor Mshahara Mpuya amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na ukosefu wa wodi ya wazazi na nyumba za watumishi hali inayosababisha wagonjwa kupata shida wakati wa usiku.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Michael Matomola ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo na kuahidi kuzitumia fedha hizo kwa kazi iliyokusudiwa huku diwani wa Kata ya Ulowa Paschal Mayengo akiwataka wananchi kushiriki Shughuli za Maendeleo.

Hii ni mara ya Pili kwa Benki ya CRDB kutoa msaada katika kijiji cha Kangeme kata ya Ulowa ambapo mara ya kwanza ilitoa Mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa Zahanati hiyo.


MATUKIO KATIKA PICHA:


MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA ELIUS KWANDIKWA MWENYE SUTI YA KIJIVU AKIWA NA MSAFARA WAKE PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA CRDB WAKIONYESHWA HATUA ILIYOFIKIA KATIKA UJENZI WA ZAHANATI YA ULOWA.

MWENYEKITI WA UMOJA WA VYAMA VYA WAKULIMA WA TUMBAKU TANZANIA (TCJE) EMMANUEL CHEREHANI MWENYE KIPAZA SAUTI AKIZUNGUMZA MBELE YA WANANCHI WA KATA YA ULOWA KUHUSU MIKAKATI YA ZAO LA TUMBAKU.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMOLA AKIONGEA NA WANANCHI WA ULOWA KUHUSU MATUMIZISAHIHI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINAZOTOLEWA NA WAHISANI PAMOJA NA SERIKALI.

WAGENI WAALIKWA,VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKIWA KATIKA MKUTANO WAHADHARA KATIKA VIWANJA VYA ZAHANATI YA ULOWA.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA KATA YA ULOWA WAKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARA.

BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA ULOWA WAKIWA WAMETULIA WAKIMSIKILIZA MENEJA WA CRDB TAWI LA KAHAMA LUTER MNENEY HAYUPO PICHANI.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA KATA YA ULOWA WAKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARA.

MWENYEKITI WA KIJIJI CHA KANGEME KATA YA ULOWA AKIZUNGUMZA JAMBO KABLA YA KUMKARIBISHA MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA MH ELIUS KWANDIKWA.

MGANGA MFAWIDHI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KANGEME KATA YA ULOWA MSHAHARA MPUYA AKISOMA RISALA KUHUSU ZAHANATI HIYO MBELE YA MGENI RASMI.

MGANGA MFAWIDHI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KANGEME KATA YA ULOWA MSHAHARA MPUYAAKIMKABIDHI RISALA MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA ELIUS KWANDIKWA.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKIWASALIMIA WANANCHI WA KATA YA ULOWA.

MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA ELIUS KWANDIKWA AKIONGEA KATIKA MKUTANO W HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KANGEME KATA YA ULOWA.

MENEJA WA BENKI YA CRDB RUTHER MNENEY AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KATA YA ULOWA KABLA YA KUKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI NANE.

MENEJA WA BENKI YA CRDB RUTHER MNENEY KULIA AKIMKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI NANE MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA ELIUS KWANDIKWA KUSHOTO,KATIKATI NI DIWANI WA KATA YA ULOWA PASCHAL MAYENGO.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WENYE T-SHIRT ZA KIJANI PAMOJA NA MWENYEKITI WA UMOJA WA VYAMA VYA WAKULIMA WA TUMBAKU TANZANIA (TCJE) EMMANUEL CHEREHANI KUSHOTO NA KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMOLA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MENEJA WA BENKI YA CRDB RUTHER MNENEY HAYUPO PICHANI.


MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMOLA KUSHOTO AKIMKABIDHI DIWANI WA KATA YA ULOWA HUNDI YA SHILINGI MILIONI NANE NA FEDHA TASLIMU SHILINGI MILIONI MOJA ILIYOTOLEWA NA MBUNGE WA JIMBO LA USHETU ELIUS KWANDIKWA.No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News