Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

ASILIMIA 95 YA WANANCHI NCHINI KUFIKIWA NA HUDUMA YA MAJI SAFI IFIKAPO 2020Serikali imesema kuwa ifikapo mwaka 2020 itahakikisha asilimia 95 ya wakazi wote wanapata huduma ya majisafi mijini ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Viwanda    hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya majisafi na majitaka inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema kuwa  Wizara yake itahakikisha kuwa lengo la kuwafikisahia wananchi wote huduma ya maji linafikiwa kwa wakati.

"Kama kuna madai yoyote ya wakandarasi na mna uhakika kuwa kazi imefanyika kwa mujibu wa mkataba yaleteni Wizarani nasi hatutakawia kuyalipa"  Alisisitiza Mhe. Aweso

Akifafanua Mhe Aweso alisema  kuwa Wizara ya Maji kamwe haiwezi kuwa kikwazo cha utekelezaji wa miradi ya maji hivyo imejipanga vyema kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika utekelezaji wa miradi ya maji.

Katika ziara hiyo Mhe. Aweso alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo na kupata taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji wilayani humo ambapo ilielezwa kuwa imeimarika hasa baada ya mitambo ya maji ya ruvu juu na ruvu chini kukamilika. 

Aidha alitembelea miradi ya maji ya Hondogo na King'azi inayotekelezwa na Manispaa, tenki la maji la Kibamba ambalo lilijengwa na DAWASA na mradi wa majitaka wa Mburahati shuleni  unaojengwa chini ya ufadhili wa Asasi ya BORDA kwa kushirikiana na Manispaa.

Moja ya changamoto inayokabili sekta hiyo ni tatizo la uvujaji wa maji ambapo Mhe. Aweso alilitaka shirika la majisafi na majitaka Dar es salaam DAWASCO kuongeza jitihada za kudhibiti tatizo la upotevu wa maji kutoka katika miundo mbinu yakusafirishia maji kwa kushirikisha wananchi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News