Header Ads

WAZIRI LUKUVI NA RC MAKONDA WAOMBWA KUMSAIDIA MJANE AMBAYE NYUMBA YAKE IMEUZWA KINYEMELA.

Siku chache  baada ya kampuni ya udalali ya Nkaya kulalamika kuipiga mnada kinyemela  nyumba  moja iliyopo Mtaa wa Kondo, Kata ya Kunduchi wilayani Kinondoni, mmiliki wa nyumba hiyo Bi Benadeta Rweyendere ameibuka na kumuomba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingilia kati.

Nyumba hiyo iliyopo Kitalu namba 239, T 110335,  Block B, imeuzwa jana na watu waliodai  ni kutoka kampuni ya udalali ya Nkaya  Company Limited, huku ikiwa na pingamizi la Mahakama Kuu ya Tanzania .

Nyumba iliyopigwa Mnada ndani ya Dakika Tano

Wauzaji hao pia wamebainika kughushi saini ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  huo  kuthibitisha  kununuliwa na mmliki mpya ambaye ni  Aisha Amour.

Akizungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo,  mmiliki wa nyumba hiyo Bi. Benadeta Rweyendera amewaambia waandushi wa habari kuwa  nyumba iliyopigwa mnada na Nkaya si  mali ya  mdaiwa Zainabu  Juma Kiswaka.

Ameeleza kwamba alinunua eneo kwa  Bi. Zainabu  mwenye ambae ana mgogoro na Nkaya,  mwaka 2015 kabla ya mgogoro huo.

Amefafanua kuwa eneo hilo limekatwa katikati ambapo upande mmoja unamilikiwa na Zainabu na upande mwingine ni wake.

"Nilijenga nyumba yangu  hapo kisha tulitenganisha maeneo kwa ukuta.Upande wangu na wa Zainabu. Ajabu watu wa Nkaya wamepauza pote  pamoja na nyumba yangu ambayo haihusiki,"alisema Bi....

Alisema yeye nu mjane  mwenye watoto watatu na tayari Nkaya wamempa notice ya siku 30 kuhama kwa sababu nyumba hiyo imeuzwa.

Awali Bi Zainabu Kiswaka alielezea kusikitishwa na tukio hilo na kwamba  nyumba imeuzwa wakati kesi bado ipo mahakamani, huku  pingamizi likiwa limewekwa toka mwaka 2017.

“Hati yangu ya eneo ilitumiwa na mataperi walighushi sahihi yangu na kukopea fedha benki ya KCB zaidi y ash.bilioni 1.6, kesi iko mahakamani nashangaa leo wanakuja kuuza nyumba. Naomba serikali inisaidie,”aslisema Zainabu.

Kwa mujibu wa shuhuda,  Shaban Mwanga, alisema mnada umefanyika ndani ya dakika tano tu na  uongozi wa serikali ya mtaa haukuhusika.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kondo , Hamis Ndonga, alithibitisha kufanyika  tukio hilo ambalo alidai ni utaperi wa wazi.

Alisema  wahusika wa kampuni ya Nkaya Company Limited wameghushi saini yake kuthibitisha uuzwaji wa nyumba wakati yeye hakuwepo hata kwenye eneo la tukio.

“Mimi sikuwepo hata katika eneo la tukio ingawa waliniletea hati ya kunijulisha kwamba wanafanya mnada wa nyumba hiyo. Nilisaini hati hiyo kuthibitisha kuipokea tu.  Lakini  sikuwa ofisini kwa sababu  leo (jana) ilikuwa siyo siku ya kazi. Tena nilishangaa kuona wanafanya mnada siku ambayo si yakazi,”alisema  mwenyekiti huyo.

Hata Moja ya Gazeti la chama Nchini Tanzania (Uhuru) limtafuta kwa njia ya simu,  Mkurugenzi wa Kampuni ya Nkaya,  Hassan Magogo, ambaye  alithibitisha kuuzwa kwa nyumba hiyo.

Alisema pingamizi lililokuwa limewekwa na mahakama lilikuwa limepitwa na wakati kwani ni la Mei 7 mwaka 2017.

“Kuhusu kughushi sahihi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, sheria  na vyombo vya sheria vipo,”alisema  mtu huyo.


Kuhusu kuuzwa kwa nyumba hiyo siku ambayo si ya kazi, Magogo , alisema mnada unaweza kufanyika siku yoyote, hata ikiwa jumamosi.
“Kama unataka njoo ofisini,”alisema.

Kati ya hati iliyotolewa na Ngaya kuhusu sababu za kuuzwa kwa nyumba hiyo, ilieleza kuwa imepewa idhini na benki ya KCB  Bank Tanzania kuuza nyumba hiyo, kwa madai iliwekewa dhamana  kwaajili ya kupata mkopo ambapo Zainabu alishindwa kurejesha sehemu ya  mkopo huo.


Hati hiyo ilieleza kuwa mmiliki wa sasa ni Aisha Amour ambaye inadaiwa alinunua kwa mnada nyumba hiyo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!