Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WATU WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA NI VIBAKA WANAHISIWA KUTUMBUKIA KWENYE KARO LA MAJI TAKA MJINI KAHAMA.

KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA  WATU WAWILI WANAODHANIWA  KUWA NI VIBAKA WANAHISIWA KUDUMBUKIA KWENYE KARO LA MAJI TAKA KATIKA MTAA WA SHUNU KATA YA NYAHANGA MJINI KAHAMA.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO AMBAPO KWA MUJIBU WA BABA MWENYE NYUMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA MAGANGA AMIAMBIA KIJUKUU BLOG KUWA TUKIO HILO LIMETOKEA MAJIRA YA SAA SABA USIKU WAKATI VIBAKA HAO WALIPOKUWA WAMEBEBANA WAKIJARIBU KUPANDA UKUTA NA NDIPO KARO HILO LILIPOTITIA.

MAGANGA AMEONGEZA KUWA USIKU WA SAA SABA ALIONA WATU WANNE HUKU WAWILI WAKIWA WAMESIMAMA PEMBENI NA WENGINE WAKIBEBANA NA NDIPO ALIPOSIKIA KISHINDO KIKUBWA CHA KARO KUTITIA .

AMEFAFANUA KUWA BAADA YA HAPO HAKUJUA KAMA WALIWEZA KUKIMBIA NA NDIPO PALIPOKUCHA ALIPOAMUA KUTOA TAARIFA KWA MAJIRANI NA WAPANGAJI WA NYUMBA HIYO.

KUFUTIA HALI HIYO JESHI LA POLISI LILIFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO KWA KUSHIRIKIANA NA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI NA KUWEKA ULINZI ENEO LA TUKIO NA KUANZA KUKAGUA KISHA KUITA GARI LA KUNYONYA MAJI TAKA ILI KUPUNGUZA MAJI HAYO.

MPAKA KIJUKUU BLOG INAONDOKA ENEO LA TUKIO HAKUNA MTU YEYOTE ALIYEONEKANA KATIKA SHIMO HILO HUKU JESHI LA POLISI LIKIWATAWANJA WANANCHI KWA AJILI YA USALA WAO.

TAARIFA NA PICHA ZAIDI ZITAKUIJIA KESHO KUPITIA KIJUKUU BLOG.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News