Header Ads

WATU 10 WAMEFARIKI BAADA YA DARAJA LA JUU KUVUNJIKA

 Daraja lenye urefu wa mita 446 nchini Colombia ambalo lilikuwa bado kwenye ujenzi limekatika na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kujeruhiwa vibaya huku wengine 11 wakiripotiwa kupotea.

Daraja hilo ambalo lilikuwa likitarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi March mwaka huu, lilijengwa kwenye eneo la mlima Chirajara kwa lengo la kuunganisha eneo hilo la Colombia kati na Mji Mkuu wa nchi hiyo uitwao Bogota.

Inaelezwa kuwa baada ya kuvunjika kwa daraja hilo, waliokuwa wanajenga walianguka mita 280 kwenda kwenye korongo jambo lililosababisha vifo hivyo na majeruhi hao.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!