Header Ads

WAPIGWA MARUFUKU KULA SAMAKI BAADA YA SAMAKI MWENYE SUMU KALI KUUZWA

Fugu

Mji mmoja nchini Japan umetangaza onyo la dharura kuzuia watu kula samaki anayejulikana kama Fugu baada ya samaki huyo mwenye sumu kali kuuzwa kimakosa.

Maduka kwenye mji wa Gamagori yaliuza mifuko mitano ya Fugu bila ya kutoa maini yake ambayo yana sumu.

Mifuko mitatu imepatikana lakini mingine miwili bado haijapatikana.

Samaki huyo ana sumu na makosa kidogo yanaweza kusababisha maafa.

Mamlaka ya mji wa Gamagori kati kati mwa Japan imetoa tahadhari na kuwashauri watu kurejesha samaki hao.

Maini ya samaki huyo na ngozi huwa na sumu kali inayoitwa tetrodotoxin na mafunzo maalumu yanahiyajika pamoja na lesini kumuandaa samaki huyo.

Hakuna dawa ya kutibu sumu ya samaki huyo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!