Header Ads

WAKULIMA WA TUMBAKU UYOGO KAHAMA WAIOMBA BODI KUONDOA KILIMO CHA MKATABA. Wakulima wa zao la Tumbaku katika chama cha msingi Uyogo Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama wameiomba bodi ya Tumbaku Tanzania kuondoa mfumo wa kilimo cha mkataba ambao unawasababisha kushindwa kuzalisha Tumbaku ya kutosha.


Akizungumza na Kijukuu Blog, mmoja wa wakulima hao AMOSI MASALA amesema kilimo cha mkataba kinawarudhisha nyuma  kimaendeleo kutokana na kupangiwa kilo za kuzalisha  na kufanya washindwe kikidhi mahitaji yao.

Nae ANDREW MNUA amesema ili kuondokana na tatizo hilo la kilimo cha mkataba ameomba bodi iwe inaingia mkataba wa mwaka mmoja na makampuni yanayonunua Tumbaku na kuangalia kipengele cha uzalishaji wa wananchi. 

Akijibu malalamiko ya wakulima hao kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku nchini HASSAN WARUSUBI, amesema atayawasilisha sehemu husika, na kuwataka wakulima kuendelea kufuata utaratibu uliopo kwa kuheshimu makisio kabla mabadiliko hayajafanyika.

Bodi ya Tumbaku Tanzania chini ya Kaimu mwenyekiti HASSAN WARUSUBI na Mkurugenzi Dkt. JULIUS NINGU wanafanya ziara katika mkoa wa kitumbaku Kahama kwa lengo la kusikiliza kero za zao hilo kutoka kwa wakulima ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!