Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WAKILI KIBATALA AJITOA KESI YA WEMA SEPETU

Wakili Peter Kibatala ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akiomba kujitoa kumuwakilisha msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Hatua hiyo imekuja leo Jumatano, baada ya shauri lililopita Desemba 12, mwaka jana, mahakama hiyo kuelezwa kuwa wakili wa Wema hajafika  na kushindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Mbali na wakili Kibatala kuomba kujitoa katika kesi hiyo,  mahakama hiyo imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumuwakilisha Wema katika kesi hiyo na kwamba aliomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayesikiliza shauri hilo, amesema kuwa amepokea barua hizo Januari 9, mwaka huu na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu, itakaposikilizwa.
 
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida  Abbas.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News