Header Ads

VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA JANUARI 15

Taarifa kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo zinaeleza kuwa Vikao vya Kamati za Bunge vinatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 15 hadi 27 January, 2018 Mjini Dodoma, hii ikiwa ni kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kumi wa Bunge.

Shughuli ambazo zimepangwa kutekelezwa katika kipindi cha vikao hivi ni pamoja na ziara za ufuatiliaji, uchambuzi wa miswada mbalimbali na kupokea maoni ya wadau, na kupokea taarifa za utendaji za wizara.

Kamati tatu za kisekta ambazo zitakuwa na jukumu la uchambuzi wa miswada ya sheria mbalimbali ni pamoja na kamati ya Katiba na Sheria, kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!