Header Ads

VIGOGO WA MGODI WA MWIME KAHAMA WAVULIWA MADARAKA KWA UBADHILIFU WA FEDHA ZAIDI YA SHILINGI MIL 260.Serikali  mkoani Shinyanga imeivunja  bodi ya Chama cha ushirika  ILINDI GOLD MINE CO-OPARATIVE SOCIETY LTD, (IGOMICO) kilichopo katika machimbo madogo ya dhahabu ya Mwime wilayani Kahama kwa  tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya milioni 260 za chama hicho.

Maamuzi hayo yamefikiwa leo na Kaimu Mrajisi msaidizi wa vyama vya  Ushirika  mkoani Shinyanga, Bi SHOSE MONYO  ambapo ameagiza pia uchunguzi ufanyike dhidi ya watuhumiwa na watakapobainika warejeshe fedha hizo.

Viongozi wanatuhumiwa  ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,  JOSEPH NALIMI, katibu mkuu wa  bodi, MARTINE BUNDALA, MESHACK  MOSES, SARAH MOSES, na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo ambapo tayari jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji baadhi yao. 

Awali wajumbe wa  IGOMICO wamedai kuwa  Viongozi wa bodi hiyo wamefanya ubadhilifu mkubwa hali iliyosababosha hasara kubwa kwa serikali na kwa wanachama.

Katika kuhakikisha majukumu ya   Ushirika huo yanaendelea,Imeundwa  Bodi  ya Muda  ya watu  sita ambayo itasimamia kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine.

Waliochaguliwa ni  ALLY MITIMINGI, ambaye amekuwa mwenyekiti na makamu wake ni ANASTAZIA MAKUNE, Katibu Mkuu ni PAUL SELEMAN, huku wajumbe ni MDALI SHABANI, MICHAEL MAZOYA  na EPHOD NSONDA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!