Header Ads

TRUMP AFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA

January 14, 2018 Daktari wa White house nchini Marekani ametangaza kuwa Donald Trump yuko katika hali nzuri kiafya, baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kwanza wa kiafya tangu achaguliwe kuw rais.

Dr. Ronny Jackson amesema kuwa uchunguzi ulichukua saa 3 ulifanywa siku ya Ijumaa alifanyiwa Trump mwenye umri wa miaka 71 na ulifanywa na madaktari wa kijeshi ulikuwa na mafanikio.

Ameahidi kutoa taarifa zaidi siku ya Jumanne. Hakuna uchunguzi wa kiakili ulipangwa kufanywa lakini kitabu kimoja cha hivi majuzi kilitilia shaka hali ya kiakili ya Rais Trump.

Kulingana na Michael Wolf, mwandishi wa kitabu cha Fire and Fury: Inside the Trump White House, ni kuwa wafanyakazi wote wa White house wanamuona Trump kama mtoto.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!