Header Ads

TANI 19 ZA SANGARA ZATIWA MIKONI MWA SERIKALI MULEBA

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Muleba imekamata tani 19 za samaki aina ya sangara wenye thamani ya Sh57 milioni ambao wamevuliwa  kinyume cha sheria katika vijiji  vilivyopo  kisiwa cha  Mazinga wilayani humo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba, Benjamini Mwakisyege amesema hayo  hii leo Jumamosi Januari 13 wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kamati hiyo kukamata  tani 7 za samaki wa aina hiyo wenye thamani ya Sh21 milioni siku ya Jumatano Janauari 10 kutoka kisiwa hicho cha  Mazinga na maeneo mengine  wilayani humo waliovuliwa kwa njia  haramu.
Mwakisyege amesema leo Ijumaa kamati hiyo pi ilikamata samaki tani 12 wenye thamani ya Sh36 milioni katika kijiji na kata ya Kagoma na kwamba samaki hao wanavuliwa kwenye vijiji  vya kata hiyo na kutoka visiwa vya Bumbire

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!