Header Ads

TAHARUKI KAHAMA,FISI WTEMBEA KWA MAKUNDI MCHANA NA USIKU.Hali ya taharuki imetanda kwa wananchi wa Kata ya Iyenze, hamashauri ya Mji wa Kahama kutokana na kundi la  wanyama aina ya fisi kuwa wanazurula mchana na usiku hivyo kuhatarisha maisha ya  wananchi wa kata hiyo.

Hayo yameelezwa na diwani wa kata  hiyo  LUCAS MAKURUMO kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya kata hiyo, kwa kipindi cha robo  ya pili ya mwaka wa fedha 2017/2018.

Amesema kutokana na  Fisi hao kuwa wanaonekana kwa makundi usiku na Mchana ni vyema halmashauri kwa kushirikiana na idara husika ikasaidia kuwasaka wanyama hao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ANDERSON MSUMBA amesema  jambo hilo wanalifanyia kazi kwa kushirikiana na mamalaka husika katika wilaya ya Kahama na kwamba wananchi watoe taarifa pindi wanapowaona wananya hao.

Kwa uapnde wake Katibu tawala wa wilaya ya Kahama TIMOTH NDANYA ameagiza utekelezaji wa haraka ili fisi hao wasileta madhara kwa wananchi na   vitu vingine vinavyotengemewa na binadamu.

Wilaya ya Kahama  imekuwa ikikumbwa na  janga la wanyama aina ya  Fisi kuvamia makazi ya watu mara kwa mara  hali ambayo inasababisha   wananachi waishi kwa hofu pamoja na kupiteeza baadhi ya mifugo yao kwa kuliwa na Fisi hao.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!