Header Ads

STEVE NYERERE: NAUMWA SANA, ALIYENIROGA ANISAMEHE

Msanii wa filamu, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kutokana na matatizo ambayo anapitia ikiwa pamoja na maradhi yake kuna watu wengi wamekuwa wakisema kuwa ameathirika na virusi vya Ukimwi.

Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha Enewz ya EATV kuwa anashangaa kwanini kila mtu anaongea lake kuhusu kuumwa kwake huku wengine wakifika mbali zaidi kwa kudai kwamba ameathirika.

“Watu wananifuatilia kutaka kujua hali yangu kwa sababu mimi ni mtu maarufu, ni jambo jema lakini kama kuna watu wamenitupia vitu vya ajabu naomba wanisamehe, mimi ni binadamu labda kuna namna watu nimewakosea,” alisema Steve. 

“Lakini nashangaa kuna watu wanadai imeathirika mmenipima, yaani kila mtu anaongea lake,”

Steve amedai kwa sasa anasumbuliwa na mbavu, miguu na tayari ameanza kupatiwa matibabu.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!