Header Ads

RAIS LIBERIA ATIMULIWA

Rais anayemaliza muda wake nchini Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ametimuliwa katika chama chake kwa tuhuma za kutomuunga mkono mgombea wake ili amrithi.

Chama chake cha Unity kinamtuhumu Bi. Ellen, kwa kuwahamasisha wananchi kutompigia kura mgombea ambaye alikuwa Makamu wa Rais, Joseph Boakai.

Aidha, chama hicho kinamtuhumu kwa kukiuka Katiba kwa madai ya kumfanyia kampeni George Weah, ambaye aligombea kupitia chama cha Coalition for Democratic Change, na kuibuka mshindi.

Weah ambaye ni mwanasoka nyota wa zamani, ataapishwa rasmi tarehe 22 mwezi huu ikiwa ni mara ya kwanza Liberia inashuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani tangu mwaka 1944

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!