Header Ads

MWANAFUNZI ALIYEPEWA MIMBA RUKWA AHUKUMIW KIFUNGO CHA MIEZI SITA JELA.

Mwananfunzi Aghata Mwananyau (19), aliyekatisha masomo akiwa kidato cha nne baada ya kupewa ujauzito, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya shilingi 300,000.
Msichana huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ,kangale, katika Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa, aliacha masomo baada ya kupewa ujauzito na Alfa Nestory (20).
Mshtakiwa huyo alishindwa kulipa faini hiyo ambapo ameanza kutumikia adhabu hiyo.
Juzi aliitwa na upande wa mashtaka kutoa ushahidi katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ambapo alitoa ushahidi wa uongo akisema aliyempatia ujauzito hakuwa mshtakiwa Nestory bali alikuwa ‘mmachinga’ aliyetokea Mbeya, tofauti na maelezo ya awali.
Ndipo Mwendesha Mashtaka, Hakimu Gwelo, alipomshtaki kwa kutoa ushahidi wa uongo, ambapo jana alifikishwa mahakamani hapo na alisomewa mashtaka hayo, na alikiri kutenda kosa hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Rugemalira, alisema amezingatia utetezi wa mshtakiwa kuwa apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mtoto mchanga mwenye umri wa miezi nane.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!