Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MTOTO ACHOMWA MOTO MIKONO KISA SUKARI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,  Jaffary Mohamed  amethibitisha kuwa wanamshikila Nyandaro Kusoya mkazi wa kijiji cha Nyang'oma kwa tuhuma za kumchoma moto mikono yote mtoto wa kaka yake, Sarah Kaela.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa  Polisi  Mkoa wa Mara amesema mtuhimiwa huyo Nyandaro Kusoya mwenye umri wa miaka 29 alimchoma moto mtoto huyo wa kaka yake, Sarah Kaela mwenye umri wa miaka mitatu kwa kile kinachodaiwa alifanya  kosa la kulamba sukari.

Bibi wa mtoto huyo Nyamata Chihoye amesema mtuhumiwa huyo Nyandaro Kusoya alimfata mjukuu wake huyo  na kuondoka naye kwa lengo la kwenda kuishi naye katika kijiji cha Nyang'oma Musoma vijijini Mkoani Mara na matokeo yake kusikia mjukuu wake amefanyiwa kitendo cha kikatili.

Aidha Kamanda Mohamed amesema wanafanya taratibu za kisheria ili kuhakikisha wanamfikisha mtuhumiwa mahakamani.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News