Header Ads

MKUU WA WILAYA KULA SAHANI MOJA NA WANAUME WANAOWAPIGA WAKE ZAO.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amepiga marufuku vitendo vya wanaume walio kwenye ndoa kupiga wake zao, akisema watakaobainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni wa madarasa ya shule ya Sekondari Tagamenda wilayani hapa, Kasesela amesema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya familia nyingi kuchukulia vitendo hivyo kama jambo la kawaida.

Alisema hadi sasa ameshawachukulia hatua za kisheria wanaume zaidi ya watatu na kuwataka wanawake kuacha kuchukulia vitendo hivyo kama sehemu ya maisha yao na kuwataka kuripoti ili waweze kusaidiwa na pia kutokomezwa kwa vitendo hivyo vya kiuonevu.

" Ninatangaza hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana ndani ya familia kama Baba na Mama hawana maelewano mazuri, na mimi sitaki kubeba dhambi za mtu yeyote atakayempiga mkewe mimi nitapambana nae," alisema Kasesela.

Hatua hiyo ya Mkuu huyo wa Wilaya ilipokelewa kwa shangwe na wakina mama wengi ambao walisema sasa amani itarejea ndani ya familia zao kutokana na wanaume wao kuwapiga hivyo sasa wanaamini furaha itakuwepo na mafanikio yatapatikana.

Pia Kasesela aliwataka wazazi hao kuwafundisha maadili yaliyo mema watoto wao ili waweze kujitunza na kuepuka maambukizi ya magonjwa ukiwemo UKIMWI.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!